PANYA WAMNYIMA RAHA RAISI WA NIGERIA AAMUA KUFANYIA KAZI NYUMBANI KWAKE

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, atalazimika kufanyia kazi zake akiwa nyumbani baada ya panya kuharibu ofisi yake iliyopo Ikulu.

Msemaji wa Rais Buhari, Garba Shehu, amesema, panya hao wameharibu samani za viyoyozi katika ofisi hiyo hivyo kiongozi huyo hawezi kufanya kazi katika ofisi mbovu ambayo itakarabatiwa kwa kipindi cha miezi mitatu.

Bw. Garba amesema, hatua ya Rais Buhari kufanyia kazi zake nyumbani hakutaathiri ufanisi wake kwa aina yoyote ile.

Rais Buhari alirejea nyumbani Nigeria Jumamosi iliyopita baada ya kukaa Jijini London nchini Uingereza kwa zaidi ya siku 100 alikokuwa akipatiwa matibabu kwa ugonjwa ambao hata hivyo haujawekwa wazi.

Comments

Popular posts from this blog

TAZAMA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI

WAZIRI ANAESHUGHULIKIA MASUALA YA AFRIKA KATIKA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA UINGEREZA AFANYA ZIARA YA SIKU MBILI NCHINI