TAZAMA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI
1
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAOFISI YA RAISTAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAATAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UCHAGUZI WA WANAFUNZI KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2017 AWAMU YAPILI (
SECOND SELECTION)
Uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwamwaka 2017 umehusisha wanafunzi
93,019
kati yao wasichana ni
37,688
na wavulana
55,331
. Wanafunzi
1,933
wakiwemo wasichana
1,132
na wavulana
801
walikosa sifaza kuchaguliwa kwa kuwa na umri mkubwa (zaidi ya miaka 25) na kukosa tahasusi.Mnamo tarehe 9 Juni, 2017 OR-TAMISEMI ilitangaza matokeo ya wanafunzi kujiungana Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa awamu ya kwanza na jumla yawanafunzi waliopangiwa ni
56,415
sawa na 60.60% ya wanafunzi wote wenye sifa,wakiwemo wasichana
25,624
na wavulana
30,791 wali.
Wanafunzi
34,727
wakiwemo
wasichana
10,932
na wavulana
23,795
hawakuchaguliwa katika awamu ya kwanza kwa kukosa nafasi. Kati ya haowanafunzi
14,768
wakiwemo wasichana
6,763 (
Sayansi
2,171
na Sanaa
4,592)
nawavulana
8,005 (
Sayansi
3,063
na Sanaa
4,942)
wamechaguliwa kujiunga na Kidatocha Tano katika awamu ya pili baada ya kupatikana nafasi zilizotokana nawanafunzi ambao hawakuripoti katika awamu ya kwanza; na kwenye shulezilizoongeza miundombinu ya Kidato cha Tano.Aidha, wanafunzi
19,959 (
wakiwemo
wasichana
4,169
na
wavulana
15,790)
hawajapangiwa shule kutokana na kukosekana kwa nafasi.Wanafunzi wote waliochaguliwa wataanza muhula wa kwanza wa masomo tarehe 24Agosti, 2017 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wotewanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati.


2
Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 08 Septemba 2017, atakuwaamepoteza nafasi. Wanafuni wote waliochaguliwa kujiunga na Kidatocha Tano,wanatakiwa ku-
download
fomu ya kujiunga na shule husika kwenye Tovuti ya OR-TAMISEMI.Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2017katika awamu ya pili pamoja na fomu za kujiunga na shule (joining instructions)inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI, www.tamisemi.go.tz
Imetolewa na:Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais
–
TAMISEMI23 Agosti, 2017

Comments
Post a Comment