KAMANDA WA KIKOSI CHA MAJINI NCHINI MAREKANI KUFUTWA KAZI

Jeshi la wanamaji la Marekani limesema kuwa litamfuta kazi kamanda Joseph Aucoin wa kikosi cha wanamaji kinachofahamika kama Seventh Fleet, kufuatia visa vya kugongwa kwa manowari za kivita maeneo ya Asia.

Mabaharia 10 bado hawajulikani waliko baada ya manowari ya USS John S McCain kugongana na meli ya kubeba mafuta karibu Singapore siku ya Jumatatu

Maafisa wa jeshi la wanamaji wanasema kuwa miili ya binadamu imepatikana ndani ya manowari hiyo ambayo kwa sasa imetia nanga katika bandari ya Singapore.
Manowari ya USS John S McCain ilikuwa mashariki mwa Singapore wakati iligongana na meli ya kubeba mafuta ya Alnic MC mapema siku ya Jumatatu.
Kisa hicho ndicho cha nne ya kugongwa kwa meli mwaka huu.

Kikosi cha Seventh Fleet chenye makao yake huko Yokosuka Japan kina karibu manowari 50 na 70 pamoja na nyambizi.

Joseph Aucoin ambaye amekuwa kamanda tangu mwaka 2015 alikuwa astaafu wiki chache zinazokuja,

Comments

Popular posts from this blog

TAZAMA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI

WAZIRI ANAESHUGHULIKIA MASUALA YA AFRIKA KATIKA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA UINGEREZA AFANYA ZIARA YA SIKU MBILI NCHINI